Pages

Saturday, March 5, 2011

Usher matatani kwa kuhusishwa na tamasha la Gadhafi.

  
Usher Rymond anasema yuko matatani baada ya kuhusishwa na tamasha la familia ya kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi.

Mapema wiki hii, wanamuziki Mariah Carey, Beyonce na Nelly Furtado walitangaza tena  kushiriki kwao katika tamasha binafsi wakitajwa kuhusishwa na familia ya Gadhafi ambayo nchi yao inampinga na iko katika uchunguzi kuhusiana na makosa ya jinai yanayomkabili kiongozi huyo.

Usher hajashiriki tamasha hilo isipokuwa anatajwa kulipwa na kushiriki tamasha la binafsi lililomshirikisha mwanamuziki Beyonce 2009.

"Niko matatani baada ya kuhusishwa na  mazingira yaliopo kwenye tamasha hilo la Nikki Beach St Bart ambalo litafanyika Uingereza" alisema Usher.

No comments:

Post a Comment